Play Store Download Pending

Play Store Download Pending

Kupakua app haikutakiwa kuwa ngumu kama vile ilivyo sasa.

·

4 min read

Kupakua (Downloading) app kutoka Google Play store inatakiwa kuwa ni kitu rahisi sana na cha moja kwa moja.Ukigusa tu "install" basi ianze hesabu zile % app iingie katika simu yako.

Nini kinapelekea app kuganda katika "Download Pending"? Kaa nami hapa leo utajifunza mengi.

1. Angalia Updates au Downloads zinazoendelea mda huo.

Mara nyingi sababu kubwa ya kukutana na download pending, ni uwepo updates ambazo zinaendelea bila wewe kujua.

Wakati mwingine ni wewe mwenyewe unakuwa umeruhusu upakuaji wa app zaidi ya moja.

Tunarekebisha vipi?

Nenda hapa:

Google Play > Menu > My apps & games.

Utaona ni apps zipi zinapakuliwa au kuwa updated. Hapo sasa gusa tu kwenye "X" upande wa kulia wa kila app.

Utakuwa umezizuia hizo updates, kisha pakua app yako moja uliyokuwa na haraka nayo.

2.Angali mtandao wako & Bando

Hii unaweza ona ni sababu isiyo na mashiko, lakini inabidi kuwa kati ya kitu cya kwanza kuangalia.

Kama una mtandao usio na nguvu basi itabaki hivyo hivyo "download pending". Toka hilo eneo lisilo na mtandao au badilisha mtandao unaotumia

Jaribu pia hata kutumia Wi-Fi kama Mobile data yako iko pole pole sana. Pia katika Play Store settings ruhusu kupakua app kwa Mobile data au Wifi (Over any Network). Ingia hapa kufanya hivyo

Settings > App download preference > Over any network

3. Je, Una Storage ya kutosha kuweza pakua hiyo app?

Kuna wengi wamekutwa na hili tatizo sababu hawakuwa na space ya kutosha.

Kawaida play store itakupa ujumbe kama space iliyobaki haitoshi, lakini jihakikishie kama ni space haitoshi au laa. Ingia

Settings > Storage

Mara nyingi huwa kama Available Space (Space iliyobaki) ni chini ya 1Gb na app unayotaka download ina kati ya 100MB ~ 1GB basi itagoma kupakua app.

Mengine ni hesabu tu ya kawaida. Huwezi kuwa na Space 1GB, alafu eti upakue app yenye zaid ya 1GB.

We Uliskia wapi? Kama ukishakuta hivyo, basi cha kufanya ni hiki.

Futa tu baadhi ya vitu kama apps usizotumia, Video & Picha usizohitaji na Baadhi ya vitu vingine unavyoweza futa

4. Restart hiyo simu.

Hakuna background updates ? Mtandao upo ? Storage Space inajitosheleza ? Bando lipo ?

Iwapo jibu ni "ndiyo" katika hayo yote basi hapo cha kufanya sasa restart tu hiyo simu tuiamshe hiyo system yako na upya. Huenda bado imelala.

5. Futa cache & data za google play store.

Yani bado upo tu hapa unasoma huu uzi? Tatizo lako hilo limekuwa sugu Grinning face with smiling eyes.

Hapo sasa cha kufanya ingia hapa:

Settings > Apps > Google Play Store > Storage

Hapo ndani ya storage Clear Cache & Data, kisha Restart simu & pakua tena app.

6. Clear Play Services

Usihofu bado haujagonga mwamba. Kama na hapo bado rudi pale kwenye Apps. Upande wa kulia juu pale kutakuwa na ( . ) tatu. Gusa pale kisha Chagua "Show System". Hapa utaweza ona apps zinazokuja na simu.

Hapa ingia Google Play Services > Storage.

Kisha clear Cache & Data, restart simu alafu jaribu tena kupakua hiyo app yako.

Kwa uhakika zaidi unaweza Clear Cache & Data za Download Manager app kabla huja restart simu.

7. Angalia kama kuna System Updates.

Wakati mwingine unahitaji tu kufanya update ya Android system yako au Security update. Kufanya hivyo, ingia settings nenda chini kabisa.

About > Software updates > Check now

Kama kuna update inahitajika. Iruhusu ipakuliwe.

Update Play Store.

Play store yenyewe pia huwa inatakiwa kuwa updated. Isipokuwa updated inaweza kuwa sababu ya matatizo hayo. Ili ku-update play store. Ingia hapa katika menu ya Play store kisha

Settings > About > Play Store version.

Kama kuna update inahitajika. Ukigusa tu "Play Store Version" uodate hiyo itaanza pakuliwa.

8. Badilisha google account iliyopo play store.

Ingia:

Settings > Accounts & Sync

Tafuta google account yako kisha itoe kwa kugusa "Remove Account".

Baada ya hapo login tena kwa account ile ile au nyingine.

9.Toa Updates za Play Store.

Hapa Baba/Mama umefika mwisho wa kamba. Pole sana. Siyo suluhisho la uhakika, lakini tufanyaje sasa?

Ingia: Settings > Apps > Google Play Store> Uninstall updates

Mwisho

USIRUHUSU mtu akwambie/kufanya FACTORY RESET bila kujaribu kutoa Updates za Play store.

Kilichobaki ni kujaribu kupakua tena app zako. Usijali kuhusu kutoa play store updates. Zitajipakua zenyewe ukifungua tena play store.Hayo yote yameshindwa tatua tatizo? Kuna njia mbadala japo si salama sana na wengi inawashinda.

Njia hiyo ni kupakua kutoka google moja kwa moja kupitia browser yako yoyote pendwa.